JINSI NILIVYOFAULU

READ MORE

1.    Jiwekee lengo moja kubwa ambalo utalifanyia kazi kila siku.

2.     Kila siku kazana kuwa bora zaidi ya jana, shindana na wewe mwenyewe na siyo mtu mwingine.

3.    Kwenye kila kipato unachoingiza, tenga asilimia 10 na weka pembeni kabla hujaanza kutumia.

4.     Asilimia 10 unayoiweka pembeni, iwekeze sehemu ambayo inazalisha zaidi.

5.     Punguza sana au acha kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama haikuingizii kipato.

6.    Usianze siku yako kwa kufuatilia habari.

7.     Amka mapema zaidi ya ulivyozoea, angalau saa moja na tumia muda huo kusali/kutahajudi, kujisomea na kufanya mazoezi.

8.     Pangilia siku yako kabla hujaianza, tafakari siku yako kabla hujaimaliza.

9.     Weka muda kwenye kujenga mahusiano yako, hasa ya wale wa karibu.

10.   Weka juhudi zaidi kwenye kazi/biashara, nenda hatua ua ziada kwa kila unachofanya.

11.   Usitoe ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba, usichukue ushauri kwa ambaye hujamwomba.

12.   Usijisumbue kuwabadilisha watu, watu huwa hawabadilishwi.

13.   Shukuru kwa kila jambo, pokea kila hali unayokutana nayo na igeuze kuwa bora.

14.   Usilalamike wala kumlaumu yeyote kwa chochote, beba jukumu la maisha yako.

15.   Fanya kilicho sahihi mara zote na siyo kilicho rahisi.

                                                ↓↓↓


 Fanya hayo kila siku kwa siku 365 za mwaka na utakuwa kufaulu kwako kutakuwa wazi kwa wengine.


Comments

Popular posts from this blog

EVERYBODY AKAE KWAKE

DEAR FUTURE WIFE